TANGAZO LA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2020/2021

TANGAZO LA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2020/2021

Chuo Kikuu cha Sayansi za Afya cha Mtakatifu Fransisko (Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Agustino Tanzania) – SFUCHAS kilichopo Ifakara, Morogoro kinapenda kuutaarifu umma kuwa UDAHILI kwa kozi ya shahada ya udakitari wa binadamu kwa mwaka wa masomo 2020/2021 utaanza tarehe 31/8/2020 hadi tarehe 25/9/2020.

SIFA ZA MWOMBAJI (Admission Requirements)

  1. Kwa muhitimu wa kidato cha sita awe na ufaulu usiopungua alama “D” katika masomo ya PHYSICS, CHEMISTRY, na BIOLOGY. Mhitimu anapaswa kuwa na pointi zisizopungua 6.0 katika masomo hayo matatu.
  2. Kwa mwombaji mwenye Stashahada ya Utabibu (Diploma in Clinical Medicine), mhusika ni lazima awe amehitimu kidato cha nne na kupata ufaulu usiopungua alama “D” katika masomo yafuatayo: Mathematics, Chemistry, Biology, Physics, na English. Pia mwombaji anapaswa awe na ufaulu usiopungua wastani wa “B” au GPA ya 3.0 katika masomo yake ya Stashahada ya Utabibu.

UOMBAJI KUPITIA MTANDAONI (Online Application)

Tembelea tovuti ya chuo www.sfuchas.ac.tz kisha ingia maombi mtandaoni (Online application) au tembelea moja kwa moja oas.sfuchas.ac.tz ili ukamilishe maombi yako.

NB: Maombi kwa kozi za stashahada (diploma) ya Ufamasia na Maabara yanaendelea kupokelewa hadi tarehe 15/9/2020.

 

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia

Afisa Udahili

St. Francis University College of Health and Allied Sciences

S. L. P 175, Ifakara, Morogoro

Barua pepe: admission@sfuchas.ac.tz au principal@sfuchas.ac.tz

Simu: +255 (0) 658 592 300 au +255 (0) 769 810 317

Kwa maelezo zaidi fika chuoni.

HOSTELI ZA KISASA NA ZENYE BEI NAFUU ZINAPATIKANA KWA WATAKAOWAHI.