TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MATOKEO YA UCHAGUZI WA UDAHILI AWAMU YA KWANZA KWA KOZI ZA AFYA KATIKA MKUPUO WA SEPTEMBA 2022/2023
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linapenda kutoa taarifa kwa umma kwamba matokeo ya uchaguzi awamu ya kwanza kwa waombaji wa programu za afya mkupuo wa Septemba 2022/2023 yametoka rasmi leo tarehe 15 Agosti, 2022. Baraza lilipokea jumla ya maombi 31,158 (wanawake 15,711 (50.4%) na wanaume 15,447 (49.6%))…